×

Fahamu Mabasi ya Kifahari Yanayotumiwa na Timu Kubwa Ulaya

Timu kubwa za soka barani Ulaya zimeendelea kuwekeza katika usafiri wa kisasa kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi, huku mabasi yao yakigeuka kuwa sehemu ya utambulisho wa klabu hizo duniani.

Mbali na ubora wa viwanja na vikosi vyao, vilabu hivyo pia vinamiliki mabasi ya kifahari yenye teknolojia ya kisasa, viti vya starehe, sehemu za burudani, WiFi pamoja na muonekano wa kuvutia wenye nembo na rangi rasmi za timu.

Mabingwa wa Hispania, Real Madrid, wanatumia basi aina ya Irizar i8 ambalo linatajwa kuwa moja ya mabasi bora kwa timu za soka duniani kutokana na ubora wake wa ndani na muonekano wa kisasa.

Kwa upande wa FC Barcelona, wao hutumia basi la MAN Lion’s Coach, huku Manchester City ya England ikitumia Volvo 9700 yenye huduma za kisasa kwa ajili ya safari za timu hiyo.

Manchester United wao wanamiliki basi aina ya Setra TopClass, wakati Liverpool FC hutumia Setra Luxury Coach inayojulikana kwa ubora wa viti na nafasi kubwa ndani ya basi.

Arsenal FC hutumia Mercedes-Benz Tourismo, huku Chelsea FC wakisafiri kwa Volvo Executive Coach inayotajwa kuwa na muonekano wa kifahari unaoendana na hadhi ya klabu hiyo ya London.

Nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) hutumia MAN Lion’s Coach, huku Olympique de Marseille wakitumia Mercedes-Benz Coach kwa safari zao za ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wa Bundesliga, Bayern Munich wanajivunia basi lao la MAN Team Bus ambalo limekuwa maarufu kwa rangi nyekundu na muonekano wa kisasa, wakati Borussia Dortmund hutumia MAN Double Decker, basi la ghorofa mbili linalovutia mashabiki wengi kila linapoonekana.

RB Leipzig wao hutumia Mercedes-Benz Travego yenye mfumo wa kisasa wa usalama na starehe kwa wachezaji.

Nchini Italia, Juventus hutumia Iveco Magelys, AC Milan wakisafiri kwa Volvo Luxury Coach huku Inter Milan wakimiliki basi aina ya Scania Touring.

Katika ligi ya Uholanzi, Ajax hutumia VDL Futura, wakati Benfica ya Ureno hutumia Irizar PB na FC Porto wakijivunia Neoplan Skyliner yenye muonekano mkubwa wa kisasa.

Mabasi hayo yameendelea kuwa sehemu muhimu ya hadhi ya klabu kubwa duniani, huku mashabiki wengi wakivutiwa si tu na mafanikio ya timu zao, bali pia muonekano wa usafiri wa kifahari unaotumiwa na vilabu hivyo.

Leave a Comment