
Mashindano ya Monaco Grand Prix mwaka 2026 yameendelea kuvuta hisia za mashabiki wa Formula One duniani baada ya kijana wa Mercedes, Kimi Antonelli, kuibuka mshindi wa mbio hizo za kifahari zilizofanyika katika mitaa ya Monaco.
Antonelli mwenye umri wa miaka 19 aliweka historia kwa kuwa dereva mdogo zaidi kushinda Monaco GP baada ya kuongoza mbio hizo kwa ustadi mkubwa licha ya vurugu za ajali, safety car pamoja na red flag zilizotokea mwishoni mwa mashindano.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Lewis Hamilton wa Ferrari huku Isack Hadjar wa Red Bull akimaliza wa tatu.
Antonelli, ameendelea kuandika historia baada ya kushinda Monaco Grand Prix 2026 na kuongeza ushindi wake wa mfululizo hadi mbio tano (5) mfululizo.
Matokeo ya Monaco GP 2026 (Top 10)
🥇 1. Kimi Antonelli (Mercedes)
🥈 2. Lewis Hamilton (Ferrari)
🥉 3. Isack Hadjar (Red Bull)
4. Oscar Piastri (McLaren)
5. Liam Lawson (Racing Bulls)
6. Arvid Lindblad (Racing Bulls)
7. Pierre Gasly (Alpine)
8. Alex Albon (Williams)
9. Esteban Ocon (Haas)
10. Fernando Alonso (Aston Martin)

Antonelli aliongoza kwa zaidi ya sekunde 30 kabla ya ajali zilizotokea katika kona ya mwisho ya mzunguko kusababisha Safety Car na baadaye red flag, jambo lililorudisha mbio upya kwa kuanza tena kutoka gridi.
Katika kuanza upya kwa mbio, Antonelli alihimili presha kubwa kutoka kwa Lewis Hamilton, lakini aliweza kuongoza tena na kujenga tofauti ya sekunde kadhaa hadi kumaliza mshindi.
Monaco GP 2026 imekuwa moja ya mbio za kukumbukwa zaidi kutokana na:
- Ushindi wa kihistoria wa Antonelli
- Ajali na red flags nyingi
- Mabadiliko makubwa ya msimamo baada ya adhabu
- Ushindani mkali kati ya Mercedes na Ferrari
