×

Sakata la Mikopo Vyuo Vikuu ya HESLB, Wanafunzi 17 Wapandishwa Kisutu

Wanafunzi17 na mhitimu mmoja kutoka vyuo nane hapa nchini wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa tuhuma za kughushi nyaraka kuonesha baba zao ni walemavu.
Wanaodaiwa wanafunzi hao ni Frank Kayamba, Sophia Macha, Clara Nyarusai, Eline Urio, Brian Assem, Loveness Mrutu Elias Kasiga, Eva Namjuzi,Silass Silass Nyasilu Magadula, Badru Lenga Aziza Bashiru, Anitha Godfrey, Cyprian Champunga, Elneth Nyagawa, Idrisa Omary, Mohamedi Mohamedi na Michael Shoide.
Wanatoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) , Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Kairuki University (KU), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).
Walifikisha jana jioni mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka 47 yakiwemo ya tuhuma za kughushi, kuwasilisha nyaraka ziliyoghushiwa na kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa kuwa walitenda makosa hayo mwaka jana wakiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tuhuma za kuingiza nyaraka za kughushi kwenye mfumo wa online loan Application and Management System (OLAMS).
Wanafunzi wote wapo nje kwa dhamana baada ya kujidhamini wenyewe kwa kutumia vitambulisho vyao. Kesi imeahirishwa hadi Juni 9,2026 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali kwa sababu upelelezi umekamilika.

Leave a Comment