×

Misri Yaandika Historia Kombe la Dunia 2026, Saudi Arabia na Tunisia Zapata Vipigo

Timu za Kiarabu zimekuwa na matokeo tofauti katika Kombe la Dunia 2026, huku Misri ikiandika historia kwa kupata ushindi wake wa kwanza kabisa katika michuano hiyo, wakati Saudi Arabia na Tunisia zikishindwa kuonyesha makali yao na kuondoka na vipigo.

Misri Yaandika Historia
Timu ya taifa ya Misri Team iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya New Zealand katika mchezo wa Kundi G uliochezwa Vancouver, Canada.

New Zealand walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Finn Surman dakika ya 15, lakini Misri walijibu kupitia Mostafa Zico kabla ya nahodha Mohamed Salah kufunga bao la pili dakika ya 67. Mshambuliaji Mahmoud Hassan Trezeguet alihitimisha ushindi huo kwa bao la tatu.

Ushindi huo umeifanya Misri kuongoza Kundi G kwa alama nne na sasa wanahitaji sare tu dhidi ya Iran ili kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Akizungumza baada ya mchezo, Salah alisema ushindi huo ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika historia ya soka la Misri na kuwapongeza mashabiki wa nchi hiyo waliojitokeza kwa wingi uwanjani.

Saudi Arabia Yapigwa na Hispania
Katika Kundi H, mabingwa wa Ulaya Spaini waliifunga Saudi Arabia  mabao 4-0.

Kijana nyota Lamine Yamal alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 10 kabla ya Mikel Oyarzabal kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu na kuifanya Hispania kuongoza 3-0 mapema. Bao la nne lilitokana na kujifunga kwa beki Hassan Al-Tambakti.

Ushindi huo umeiweka Hispania kileleni mwa Kundi H ikiwa na alama nne baada ya michezo miwili.

Iran Yaizuia Belgium
Katika mchezo mwingine wa Kundi G, Ubelijiji  ililazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Iran.

Belgium walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya Nathan Ngoy kutolewa kwa kadi nyekundu, huku Iran ikionyesha nidhamu kubwa ya ulinzi na kuondoka na pointi muhimu.

Japan Yaiondoa Tunisia
Nayo Japan iliendeleza kiwango bora kwa kuichapa Tunisia mabao 4-0.

Ushindi huo umeisogeza Japan karibu zaidi na hatua ya 32 bora huku ukiiondoa Tunisia rasmi kwenye mashindano hayo.

Kocha wa Japan, Hajime Moriyasu, alisema ameridhishwa na namna kikosi chake kilivyocheza licha ya kukosa huduma za nyota wao Takefusa Kubo kutokana na majeraha.

Leave a Comment