×

Exim Bank yaboresha usalama na elimu Zanzibar kupitia Exim Cares

Benki ya Exim Tanzania kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii (Exim Cares), imeendelea kuboresha maisha ya wananchi Zanzibar kwa kutekeleza miradi inayolenga sekta za usalama na elimu.

Baada ya kufungua Tawi la Paje, benki hiyo ilikabidhi samani za ofisi kwa Kituo cha Polisi Paje pamoja na madawati 80 kwa Shule ya Msingi Paje, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Exim Bank Tanzania, Stanley Kafu, alisema benki hiyo inaamini kuwa uwekezaji katika elimu na maendeleo ya jamii ni msingi wa maendeleo endelevu.

Madawati hayo yanatarajiwa kunufaisha zaidi ya wanafunzi 250 kila mwaka, huku msaada wa samani ukiimarisha uwezo wa Kituo cha Polisi Paje kutoa huduma bora kwa wakazi wa eneo hilo.

Miradi hiyo ni sehemu ya mkakati wa Exim Bank wa kuimarisha maendeleo ya jamii kupitia elimu, uwezeshaji wa wananchi na ushirikiano wa muda mrefu na jamii za Zanzibar, sambamba na utoaji wa huduma za kifedha.

 

Leave a Comment