×

Shigongo: Serikali Iendelee Kufungua Fursa za Kiuchumi kwa Vijana – Video

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amesema ataendelea kuishauri na kuibana Serikali kuhakikisha inaweka mazingira bora yatakayowawezesha vijana wa Kitanzania kutambua na kutumia ipasavyo fursa mbalimbali za kiuchumi ili waweze kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.

Shigongo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika maadhimisho ya miaka mitano ya Young CEO Roundtable Africa, ambapo alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwawezesha vijana kiuchumi.

Alitaja miongoni mwa hatua hizo kuwa ni marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma, ambayo sasa yanatoa kipaumbele kwa wazawa kushiriki zabuni za biashara zenye thamani ya hadi shilingi bilioni 50, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kampuni za kigeni zilikuwa zikinufaika zaidi.

Mbali na hilo, Shigongo amesema Serikali imeendelea kufungua milango ya fursa kwa vijana kupitia uwezeshaji wa mitaji, akibainisha kuwa Rais Dkt. Samia ametenga shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kukuza mitaji yao na kuimarisha shughuli za kiuchumi.

Amesisitiza kuwa jukumu la Serikali ni kuweka mazingira rafiki yanayowezesha wananchi kufanikiwa, huku akieleza kuwa mafanikio ya mtu yanategemea namna anavyotumia fursa zinazotolewa.

> “Kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira ya watu kufanikiwa, lakini suala la kufanikiwa linabaki kuwa jukumu la mtu binafsi,” amesema Shigongo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)

Leave a Comment