×

Omary Katanga wa Efm asherehekea miaka 38

Omary Katanga (1)

Omary Katanga akifungua shampeni kama ishara ya kujipongeza.

Omary Katanga (2)

Mashabiki wakigongesheana ‘cheers’.

Omary Katanga (3)

Katanga akikata keki.
Omary Katanga (4)

…Akiitambulisha timu nzima ya watangazaji wenzake wa Sports Headquarter ya EfM.

Omary Katanga (5)

…Akionyesha website yake jinsi inavyofanya kazi.

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Sports Headquarter kinachorushwa kupitia kituo cha Redio cha EFM, Omary Katanga ‘Mlinda Mlango’,  amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 38 alipodondosha pati ya nguvu usiku wa kuamkia jana katika Ukumbi wa Klabu ya Masai uliyopo Mwananyamala Jijini Dar.

Pati hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali na wafanyakazi wake kutokea EfM, ilisheheni vivutio kibao ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa keki yenye taswira ya uwanja wa mpira na goli likimuonesha kipa akiokoa mchomo, alama iliyotajwa kuwa na maana ya mlinda mlango, jina ambalo hulitumia kupitia kipindi hicho.

Mbali na sherehe hiyo, mtangazaji huyo alizindua rasmi Website yake ya michezo, www.katanga.co.tz na kuwataka wapenzi wa habari hizo kuitembelea kwa habari mpya za kila siku.

(Picha/Chande Abdallah/GPL)

 

Leave a Comment