×

RC Chalamila Akutana na Ujumbe Kutoka Jiji la Yokohama-Japan

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 14, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Jiji la Yokohama-Japan ofisini kwake Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila akiwa na ujumbe huo ukiongozwa na Bw Takashi Yanagisana alipata wasaa wakujadili masuala mbalimbali ya mashirikiano ya kielimu, utamaduni, michezo, mazingira na Biashara, ambapo kupitia mazungumzo yao wamekubaliana kuendeleza mashirikiano kwa masilahi mapana ya wananchi wa Jiji la Yakohama-Japan na Dar es Salaam-Tanzania

Ifahamike kuwa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Diplomasia na mataifa mbalimbali Duniani, leo matunda ya juhudi hizo tunashuhudia ambayo yanakwenda kuchochea makuzi makubwa ya uchumi wa Tanzania.

Leave a Comment