×

Jacqueline Wolper Afichua Tabia za Kajala, Aunty Ezekiel na Irene Uwoya

Staa wa filamu za Bongo na mfanyabiashara, Jacqueline Wolper.

Staa wa filamu za Bongo na mfanyabiashara, Jacqueline Wolper, amefunguka kuhusu tabia za marafiki zake wa karibu akiwemo Kajala Masanja, Aunty Ezekiel na Irene Uwoya, akieleza jinsi kila mmoja alivyo katika maisha ya kila siku.

Akizungumza, Wolper amesema Kajala ni mtu mwenye upole, huruma na pia ana ukali pale hali inapohitaji.

Kuhusu Aunty Ezekiel, amesema ni mwanamke mpambanaji, anayependa kufuatilia yanayoendelea kwa watu, hupenda kupiga stori na ni mwenye huruma na upekee wake.

Irene Uwoya, Wolper amesema ana hasira za haraka, lakini ni mtu mwenye upendo mkubwa na anayezingatia sana ibada.

Mbali na hilo, Wolper ameeleza kuwa yeye na marafiki zake hao hukosana mara kwa mara, lakini hawadumu kwenye tofauti zao kwa sababu husuluhisha haraka.

“Sisi tunasusa wote na tunarudi haraka,” amesema Wolper.

Aidha, amekiri kuwa watu wenye ukaidi mkubwa katika kundi lao ni yeye mwenyewe na Irene Uwoya.

Katika mazungumzo hayo, Wolper pia amesema anapenda sana kupika, akieleza kuwa mapishi ni moja ya mambo anayoyafurahia zaidi katika maisha yake ya kila siku.

Mashabiki wanaweza kufuatilia mahojiano hayo kamili leo Ijumaa kupitia Maisha Magic Bongo (Channel 160) ndani ya DStv Tanzania, kuanzia saa 2:00 usiku.

Leave a Comment