
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, amefika kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kufuatilia mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na mawakili wa Tundu Lissu dhidi ya mamlaka ya Gereza la Ukonga kuhusu suala la haki ya faragha.
Kufika kwa Heche mahakamani kunakuwa baada ya muda mrefu tangu mara yake ya mwisho kuonekana hadharani mahakamani, kabla ya kuanza kwa ziara zake za kudai Katiba Mpya na kampeni ya “Free Tundu Lissu.”

Kesi hiyo inahusu madai ya mawakili wa Lissu kupinga hatua zinazodaiwa kuathiri haki ya faragha katika mawasiliano na taratibu za kumtembelea mteja wao akiwa gerezani.





