
Tarehe 1 Agosti 2026 itaingia kwenye historia ya michezo ya mapambano wakati UFC itakapofanya tukio lake la kwanza kabisa nchini Serbia. Katika tukio hilo la kipekee, Meridianbet itashiriki kama Mshirika Rasmi, ikiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini humo.
Meridianbet ilianzishwa nchini Serbia mwaka 2001 na imekua kuwa moja ya kampuni zinazoongoza katika sekta ya michezo ya kubashiri na kasino mtandaoni. Ushirikiano huu na UFC unaonesha hatua nyingine muhimu katika safari ya kampuni ya kuendelea kuimarisha uwepo wake katika matukio makubwa ya kimataifa.
Kupitia ushirikiano huu, chapa ya Meridianbet itaonekana katika maeneo mbalimbali ya tukio, ikiwemo ndani ya Belgrade Arena, kwenye matangazo rasmi ya UFC, matangazo ya video yatakayooneshwa ukumbini, pamoja na kampeni za kidijitali na mitandao ya kijamii. Hii itaifanya Meridianbet kuonekana na mamilioni ya mashabiki wa UFC duniani kote.
Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Meridian Holdings Inc. (NASDAQ: MRDN), William Scott, alisema:
“Serbia ndiyo ilipoanzia safari ya Meridianbet miaka 25 iliyopita. Kuwa sehemu ya tukio la kwanza la UFC kufanyika nchini humo ni heshima kubwa na hatua muhimu katika historia ya kampuni yetu.”
Kwa miaka mingi, Meridianbet imeendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo kupitia udhamini wa matukio mbalimbali ya kimataifa na ya ndani. Ushirikiano huu na UFC unaimarisha dhamira ya kampuni ya kuendelea kuunga mkono michezo na kuwapatia mashabiki uzoefu wa kipekee wa burudani.
Mbali na ubashiri wa michezo, Meridianbet pia inatoa michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni yenye teknolojia ya kisasa na odds zenye ushindani kwa matukio makubwa ya michezo duniani. Wateja wanaweza kujiunga kwa urahisi kupitia tovuti ya Meridianbet au kwa kupiga *149*10# na kuanza kufurahia huduma mbalimbali zinazotolewa.
Kwa wapenzi wa UFC na michezo mingine ya kimataifa, Meridianbet inaendelea kuwapa fursa ya kubashiri matukio makubwa duniani kupitia jukwaa salama, la kisasa na lenye huduma bora kwa wateja.
Tukio la UFC Fight Night Belgrade litakalofanyika tarehe 1 Agosti 2026 linatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki ukumbini pamoja na mamilioni ya watazamaji duniani. Kwa Meridianbet, ushirikiano huu ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya mafanikio na uthibitisho wa azma yake ya kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza michezo na burudani duniani.