
Mrembo wa Marekani, Jordyn Lucas, ametimiza ndoto yake ya muda mrefu baada ya kupata nafasi ya kukutana na rapa maarufu Drake.
Baada ya kukutana na msanii huyo, Jordyn anadaiwa kuondoka na zawadi ya dola 25,000 sawa na Sh milioni 66, pamoja na mkoba wa kifahari aina ya Birkin ambao alipewa na Drake.
Jordyn alionekana kufurahishwa na tukio hilo na kueleza hisia zake kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiambatanisha na video yao baada ya kukutana. Katika ujumbe huo, alionyesha mahaba ya kipekee kwa msanii huyo.

Jordyn alisema: “Mume wangu, mpenzi wangu, nguzo yangu ya maisha. Nimesubiri maisha yangu yote kwa ajili ya wakati huu na sasa imethibitishwa… tunastahili kuwa pamoja. Asante kwa Birkin yangu na dola 25,000, dada yangu.”
Kauli hiyo imezua gumzo mitandaoni, huku Jordyn akionekana kuufurahia sana mkutano wake na Drake pamoja na zawadi hizo anazodai kupewa na rapa huyo.