The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Jeshi la Ecuador yaanguka na kuua 22

0

ecuador

NDEGE ya Jeshi la Ecuador imeanguka katika misitu ya Amazon na kuua watu wote 22 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, Rais wa nchi hiyo, Rafael Correa ameeleza.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya kutoa taarifa za ndege hiyo kupata ajali, rais huyo aliandika: “Hakuna majeruhi yeyote”.

Watu 19 kati ya waliopoteza maisha walikuwa ni wanajeshi wa Ecuador waliokuwa wakisafiri kwa ajili ya mazoezi ya kuruka kwa parachuti, pia kulikuwa na marubani wawili pamoja na fundi mmoja.

Ndege hiyo iliyotengenezwa nchini Israel ilidondoka jana katika Jimbo la Pastaza.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Leave A Reply