×

Vazi nalo lina hadhi yake ni vizuri kujisitiri

Purchase this image at http://www.stocksy.com/49627

Asalam alaikum wapenzi wasomaji wangu, hakika naendelea vema na ujenzi wa taifa kama kawa kwa hilo namshukuru Mungu. Bila shaka na nyie mko salama Mungu aendelee kuwapa afya njema ili tuungane kwenye maujuzi kama kawa.
Leo nimekuja na mada ambayo hakika itawagusa akina mama wengi kwani tunakoelekea ni kujisahau na siyo uzungu kama wengi wanavyodhani.

Wanawake wengi hawajui kuwa vazi fulani lina hadhi yake mbele ya mwanaye, mkwe na hata mumewe. Wanavaa vazi lolote mbele ya wote hao niliowataja.
Akina mama mliojisahau kwa hili leo nimeamua kuja na mada hii ili kuwakumbusha kuwa wakati mwingine ni aibu kubwa kukuta umevaa kimini mbele ya mkweo yaani mume wa mtoto wako.

Hivi wewe ukivaa kimini na mwanao akavaa kimini mbele ya mumewe nani anadharaulika hapo au mkikutana na watu huoni kuwa mumeo atapata tabu ya kukutambulisha kwa sababu wote mtaonekana wake zake?
Hiyo haitoshi, unakuta mwanamke anavaa kimini akiongozana na mtoto wake wa kiume hivi huoni kuwa unamdhalilisha mwanao? Akiulizwa hili jimama lako linakulea utakasirika au utasema watu mtaani hawana adabu?

Kwa mifano hii bila shaka msomaji wangu unanielewa nataka kuongea nini, siku hizi uzungu umekithiri sana majumbani kwetu kiasi kwamba wamama wanavaa kila nguo, hivi niwaulize uafrika wetu umeenda wapi? Kwa nini tunapishana na maadili yetu?
Mkweo akikutongoza kwa sababu kaona paja lako utakasirika kweli? Umesha-ambiwa wanaume wana udhaifu ambao husababisha kumtaka kimapenzi mwanamke yeyote aliyekamilika sasa kwa wewe kujira-hisisha unategemea nini? Tujiheshimu wamama.

Kum-buka kuna vazi unaloweza kuvaa mtaani, lakini usiligeuze vazi la mumeo nyumbani ndiyo ukamvalia hata mwanao, ukiwa na mume ruksa hata kukaa upendavyo lakini nakusihi kuheshimu watu wengine ambao hawastahili kuona maungo yako.

Juzi baada ya kutoa mada iliyopita nilipokea ujumbe wa msomaji wangu wa kiume ambaye aliamua kufunguka huku akiomba ushauri kwangu kuwa, mama mkwe wake si mzee sana kwa haraka ukikutana naye akiwa ameongozana na mwanaye unaweza kusema ni dada yake.

Lakini cha kushangaza amekuwa akivaa mavazi ya mitego kumzidi hata mwanaye kitendo ambacho si sahihi kwani anamtega.

“ Kuna wakati nakuwa nimekaa sebuleni mama naye anakuja na kukaa na mimi tena kihasara, najikuta sina uhuru na nyumba yangu kwani muda mwingi nakaa chumbani, akiondoka ndiyo najiachia,” alisema msomaji huyo.
Kwa hali hii huoni kama wanawake tunajidhalilisha jamani mpaka msomaji ameamua kutuma ujumbe kwangu amechoshwa na tabia hiyo ambayo kiukweli siyo nzuri.

Leave a Comment