×

Simba Yamtambulisha Ismail Mgunda Akitokea Mashujaa FC

Klabu ya Simba leo Agosti 15, 2026 imemtambulisha rasmi mshambuliaji Ismail Mgunda kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Mgunda, mwenye umri wa miaka 31, amejiunga na Simba akitokea Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania anatarajiwa kuongeza nguvu na ushindani katika safu ya ushambuliaji ya Simba, ambayo inaendelea kujenga kikosi imara kuelekea msimu mpya 2026/27.

Leave a Comment