×

SportPesa Yaungana na Tanzania Rugby Union Kukuza Rugby Nchini

Dar es Salaam, Agosti 24, 2026 — SportPesa imetangaza ushirikiano na Tanzania Rugby Union (TRU) kwa ajili ya kusaidia maendeleo na ukuaji wa mchezo wa rugby nchini Tanzania.

Kupitia ushirikiano huo, SportPesa imekuwa Mdhamini Mkuu wa Mashindano ya Taifa ya Rugby Saba, yatakayojulikana kama SportPesa National Saba Circuit 2026.

Aidha, kampuni hiyo itakuwa Mshirika Rasmi wa Kipekee wa Kamari wa mashindano hayo, katika makubaliano yatakayodumu kwa kipindi cha miezi mitano.

Ushirikiano huo unalenga kuongeza mwonekano wa mashindano, ushirikishwaji wa mashabiki, maudhui ya kidijitali, shughuli mbalimbali za uwanjani pamoja na kusaidia maendeleo ya vipaji vya rugby nchini.

Mbali na mashindano ya SportPesa National Saba Circuit 2026, SportPesa pia itaunga mkono Timu ya Taifa ya Wanaume, Twiga Kings, katika safari yake ya kwenda Afrika Kusini kushiriki mashindano ya Obaro 7s yatakayofanyika mwezi Oktoba.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, amesema kampuni hiyo inaamini uwekezaji katika michezo ni muhimu kwa ajili ya kujenga sekta imara ya michezo.

Amesema rugby ina nafasi kubwa ya kukua nchini Tanzania kutokana na shauku iliyopo miongoni mwa mashabiki na jamii inayouzunguka mchezo huo.

Kwa upande wake, Rais wa Tanzania Rugby Union, Jacob Jonas, amesema ushirikiano huo umefika wakati muhimu kwa maendeleo ya rugby nchini.

Amesema msaada huo utawezesha kuimarisha Mashindano ya Taifa ya Rugby Saba na kutoa fursa zaidi kwa wachezaji, makocha na vipaji chipukizi kuendeleza uwezo wao.

Jonas pia amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa mashabiki katika kukuza rugby, akisema maendeleo ya mchezo huo yanahitaji kujenga pamoja na jamii inayouzunguka.

Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza fursa za ushindani kwa wachezaji wa ndani huku ukiipa rugby ya Tanzania nafasi zaidi ya kuonekana katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Leave a Comment