
Yanga SC leo Agosti 24, 2026 inatarajiwa kushuka dimbani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 12:00 jioni.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga ikilenga kuendelea na mwenendo mzuri katika msimu huu, wakati JKT Tanzania ikisaka matokeo mazuri dhidi ya mabingwa hao.
Akizungumzia mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa muda kuona timu yao ikicheza katika uwanja huo.
“Mashabiki wameusubiri kwa muda mchezo huo na sasa siku imefika ya kuiona timu yao ikicheza katika Uwanja wa KMC,” amesema Ali Kamwe.
Aidha, Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kukata tiketi kupitia simu zao ili kuepuka usumbufu wakati wa kuingia uwanjani.
Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi KMC Complex kushuhudia mchezo huo, huku klabu ikiwataka kufanya maandalizi mapema kwa kukata tiketi kabla ya kwenda uwanjani.
Mchezo huo unaongeza hamasa katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, huku macho ya mashabiki yakielekezwa KMC Complex kusubiri kuona nani ataibuka na pointi tatu.
Stori na Na Haika Urio | GPL – TUDACO
