×

Willy Nkya Aifikia Uhuru Peak, YAS Yawawezesha Kuendelea Kuwasiliana na Dunia

Kilimanjaro — Miaka tisa baada ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza, mtangazaji wa redio Willy Nkya amepanda tena mlima huo, safari hii akiwa na jukumu la kuripoti matukio mbalimbali kila siku akiwa katika kilele cha juu zaidi barani Afrika.

Nkya, ambaye alipanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza mwaka 2017, muda mfupi baada ya kumaliza chuo, amesema safari yake ya mwaka huu imekuwa tofauti kwa namna kadhaa, ikiwemo uzoefu, maandalizi ya mwili na upatikanaji wa mawasiliano.

Amesema safari hii alipanda akiwa na uzoefu zaidi pamoja na maandalizi ya kutosha ya mwili na uelewa wa namna ya kukabiliana na uchovu, baridi na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea kadri mtu anavyopanda mlima.

Hata hivyo, tofauti kubwa zaidi kwake ilikuwa ni mawasiliano, kwani safari hii aliweza kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kikazi katika maeneo mengi ya mlima.

Akiwa safarini, Nkya alitakiwa kurekodi na kutuma video, sauti, picha na taarifa mbalimbali kwa ajili ya matangazo ya redio na mitandao ya kijamii.

Amesema mtandao wa Yas ulimwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake katika maeneo mengi aliyopita kuelekea kileleni, huku pia akiendelea kuwasiliana na familia na marafiki.
“Tofauti na mwaka 2017 ambapo mawasiliano yalikuwa ya shida, safari hii mambo yalikuwa tofauti. Nimeweza kutuma video, picha, sauti na kuwasiliana bila matatizo na watu wangu wa karibu,” amesema Nkya.

Akielezea changamoto za safari hiyo, Nkya amesema kupanda Mlima Kilimanjaro si jambo rahisi kutokana na mazingira magumu yanayohusisha baridi kali, uchovu na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Kupanda Mlima Kilimanjaro si mchezo. Kuna wakati unahisi kabisa uko kwenye dunia nyingine. Mtandao wa viwango wa Yas, ambao unapatikana vizuri kabisa katika maeneo mengi ya mlima tuliyopita, umenisaidia kuendelea kutimiza majukumu yangu ya kazi bila shida,” amesema.

Aifikia Uhuru Peak

Nkya aliendelea na safari hiyo hadi kufika Uhuru Peak, yenye urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari, ikiwa ndiyo kilele cha juu zaidi barani Afrika.

Amesema safari ya mwaka huu imempa mtazamo tofauti na ile ya miaka tisa iliyopita, hasa kutokana na namna mawasiliano yalivyorahisisha utekelezaji wa majukumu yake katika mazingira magumu ya mlima.
“Kwangu hii ndiyo maana ya Mtandao wa Viwango, mtandao unaokuwezesha kuendelea kufanya kile unachotaka kufanya hata ukiwa katika safari yenye changamoto. Nimepanda na Yas hadi Uhuru Peak na nimeendelea kuwasiliana na dunia,” amesema.

Kwa Nkya, kufika Uhuru Peak hakukuwa tu mwisho wa safari, bali pia ni ujumbe kuhusu umuhimu wa kila mtu kuwa na kilele anachotamani kukifikia katika maisha yake.
“Kila mmoja wetu ana kilele anachopanda katika maisha yake. Cha kwangu safari hii kilikuwa Uhuru Peak.”

Safari hiyo imeonyesha pia namna teknolojia ya mawasiliano inavyoweza kuwa sehemu ya safari za changamoto, ikimuwezesha mtu kuendelea kufanya kazi, kuwasiliana na wapendwa wake na kushirikisha wengine uzoefu wake hata akiwa katika maeneo magumu kufikika.

Leave a Comment