
MONACO – Droo ya hatua ya Ligi ya mabingwa (league phase ya UEFA Champions League) msimu wa 2026/27 imefanyika usiku wa kuamkia leo Agosti 28, 2026 mjini Monaco, huku timu 36 zikijua wapinzani wao katika hatua hiyo ya mashindano.
Kwa mujibu wa mfumo mpya wa mashindano hayo, kila timu itacheza jumla ya mechi nane dhidi ya wapinzani tofauti, nne nyumbani na nne ugenini. Timu hizo zimegawanywa katika pots nne, huku kila timu ikipangiwa wapinzani wawili kutoka kila pot.
Miongoni mwa mapambano yanayotarajiwa kwa hamu kubwa ni kati ya Barcelona na Manchester City. Barcelona pia imepangwa kukutana na Paris Saint-Germain (PSG), Aston Villa, Sporting CP, Feyenoord, Galatasaray, Como na Sabah.
Barcelona itamkaribisha Manchester City nyumbani, kabla ya kusafiri kwenda Paris kukutana na mabingwa watetezi, PSG. Pia itakuwa na safari kwenda Uturuki kucheza dhidi ya Galatasaray na Azerbaijan kukutana na Sabah.
Kwa upande mwingine, Atlético Madrid imepangiwa kukutana na wapinzani wakubwa, akiwemo Bayern Munich, Liverpool na Manchester United, jambo linalofanya ratiba yake kuwa miongoni mwa zinazotarajiwa kwa hamu kubwa katika hatua hiyo.
Mabingwa watetezi, PSG, wataingia msimu huu wakiwa na lengo la kutetea taji lao baada ya kuifunga Arsenal kwa mikwaju ya penalti katika fainali ya msimu uliopita.
Hatua ya league phase ya Champions League msimu wa 2026/27 itaanza Septemba 8, 2026, huku timu nane zitakazomaliza katika nafasi za juu kwenye msimamo zikifuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.
RATIBA YA LIGI YA MABINGWA ULAYA 2026/27
Hatua ya League Phase
-
Mechi za 1: 8–10 Septemba 2026
-
Mechi za 2: 13–14 Oktoba 2026
-
Mechi za 3: 20–21 Oktoba 2026
-
Mechi za 4: 3–4 Novemba 2026
-
Mechi za 5: 24–25 Novemba 2026
-
Mechi za 6: 8–9 Desemba 2026
-
Mechi za 7: 19–20 Januari 2027
-
Mechi za 8: 27 Januari 2027
Hatua ya Mtoano
-
Play-off: 16/17 na 23/24 Februari 2027
-
Hatua ya 16 Bora: 9/10 na 16/17 Machi 2027
-
Robo Fainali: 6/7 na 13/14 Aprili 2027
-
Nusu Fainali: 27/28 Aprili na 4/5 Mei 2027
-
Fainali: 5 Juni 2027, Estadio Metropolitano, Madrid.
WAPINZANI WA TIMU KUU
Barcelona
-
Manchester City
-
PSG
-
Aston Villa
-
Sporting CP
-
Feyenoord
-
Galatasaray
-
Como
-
Sabah
Manchester City
-
PSG
-
Barcelona
-
Sporting CP
-
Porto
-
Napoli
-
RB Leipzig
-
AEK Athens
-
Lens
PSG
-
Barcelona
-
Manchester City
-
Roma
-
Aston Villa
-
Galatasaray
-
Villarreal
-
Slovan Bratislava
-
Como
Real Madrid
-
Arsenal
-
Inter Milan
-
PSV
-
Roma
-
RB Leipzig
-
Shakhtar Donetsk
-
LASK
-
AEK Athens
Atlético Madrid
-
Bayern Munich
-
Manchester United
-
Liverpool
-
PSV
-
Fenerbahçe
-
Bodø/Glimt
-
Viking
-
Stuttgart
Bayern Munich
-
Arsenal
-
Atlético Madrid
-
Manchester United
-
Real Betis
-
Bodø/Glimt
-
Lille
-
Slavia Prague
-
Viking Stavanger
Liverpool
-
Inter Milan
-
Atlético Madrid
-
na wapinzani wengine sita waliopangwa kwenye droo.
Arsenal
-
Real Madrid
-
Bayern Munich
-
Borussia Dortmund
-
Real Betis
-
Lille
-
Napoli
-
Slavia Prague
-
Sabah
MANCHESTER UNITED – CHAMPIONS LEAGUE 2026/27
- Bayern Munich — Nyumbani
- Atlético Madrid — Ugenini
- AS Roma — Nyumbani
- Sporting CP — Ugenini
- RB Leipzig — Nyumbani
- Villarreal — Ugenini
- Sabah FC — Nyumbani
- Como — Ugenini
Stori na Ashura Karimu | GPL- TUDACO