×

Video: Kesi ya Lissu Yaahirishwa, Mnyika Kuendelea Kudodoswa Kesho

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi kesho Septemba 2, 2026, huku Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, akitarajiwa kuendelea kujibu maswali kutoka upande wa Serikali.

Katika hatua za mwisho za mwenendo wa kesi leo, Mnyika alikabiliwa na maswali kuhusu uelewa wake wa sheria, majukumu yake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA, pamoja na kauli na msimamo wa chama kuhusu uchaguzi na vurugu.

Wakili wa Serikali, Nzengeli, alimuuliza Mnyika kama yeye ni mtaalamu wa sheria, ambapo alijibu kuwa si mtaalamu wa sheria.

Mnyika pia alikataa kuwa hana uwezo wowote wa kuchambua nyaraka, akisema anaweza kuchambua mambo kwa uelewa wake, ingawa baadaye alikiri kuwa hana utaalamu wa kisheria.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU DEMOKRASIA

Katika dodoso hilo, Mnyika alieleza kuwa endapo mtu anaamini uchaguzi ni wa haki na uhuru, lakini CHADEMA ina msimamo tofauti, mtu huyo anaweza kutokubaliana na msimamo wa chama.

Alisema kutokubaliana na msimamo wa CHADEMA ni suala la maoni ya mtu binafsi.

Wakili Job Mrema naye aliendelea kumuuliza Mnyika maswali akitumia Kamusi Kuu ya Kiswahili, Toleo la Tatu la mwaka 2022, katika kutafuta maana ya baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye ushahidi.

Mnyika alithibitisha kuwa kamusi hiyo ni rasmi, ingawa si nakala pekee inayoweza kutumika kutoa tafsiri ya Kiswahili.

Mrema alimuuliza Mnyika kuhusu majukumu yake kama Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Mnyika alisema jukumu lake ni kusimamia shughuli zote za kila siku za chama.

Alipoulizwa kama ameshindwa kutaja majukumu yake katika baadhi ya maswali yaliyoulizwa awali, Mnyika alikanusha na kusema amejibu maswali mengi, isipokuwa machache ambayo yalihitaji uelewa zaidi.

Mnyika pia alikanusha madai kwamba nafasi yake ya Katibu Mkuu imekuwa ya kusaidiwa au kwamba amekuwa akibebwa na Mwenyekiti wa CHADEMA.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU “FUJO”

Katika sehemu nyingine ya dodoso, Mrema alimuuliza Mnyika maana ya neno “fujo.”

Mnyika awali alijibu kwa kusema, “Fujo ni fujo,” lakini baada ya kuombwa kueleza maana hiyo kwa mujibu wa kamusi aliyokuwa nayo, alisema fujo ni hali ya kutokuwepo kwa utaratibu mzuri au mpango, pamoja na hali ya ghasia na machafuko.

Wakili Mrema alimuuliza Mnyika kama kauli iliyotolewa na Lissu Aprili 3, 2025 kwamba “ataleta fujo” na “atakinukisha” ilikuwa ni fujo yenyewe.

Kutokana na muda, upande wa Serikali uliomba suala hilo liendelee kesho, na Jaji akaelekeza kuwa swali hilo litashikiliwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

“SIFAHAMU MIPANGO YA CHADEMA KUHUSU VURUGU”

Katika dodoso jingine, Wakili Katuga alimuuliza Mnyika kuhusu madai ya kuwepo kwa mipango ya vurugu kabla na wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mnyika alisema hafahamu mipango hiyo.

Alipoulizwa kuhusu madai kwamba baadhi ya wanachama waliwahi kuzungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kulikuwa na mipango iliyopangwa na kuratibiwa na chama, Mnyika alisema hafahamu.

Pia alisema hafahamu madai ya kuwepo kwa mifumo maalumu ya mawasiliano ambayo ingetumika iwapo mitandao ya simu ingezimwa.

MNYIKA AULIZWA KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

Katuga alimuuliza Mnyika kama anafahamu kuwa vurugu za siku ya uchaguzi zilidaiwa kuwa zilipangwa na kuratibiwa.

Mnyika alisema alisikia kuhusu madai hayo.

Alipoulizwa kuhusu watu waliokamatwa kuhusiana na vurugu hizo, Mnyika alisema anafahamu kuwa baadhi yao walikamatwa na baadaye wakaachiwa.

Hata hivyo, alipohojiwa kuhusu madai kwamba watuhumiwa walifanya fujo kituoni kutokana na kauli za kiongozi wao, Tundu Lissu, Mnyika alisema hafahamu.

LISSU AOMBA MWENENDO WA KESI

Baada ya kesi kuahirishwa, Tundu Lissu aliomba apewe mwenendo wa kesi ili aweze kuusoma akiwa aliko.

Upande wa Serikali unatarajiwa kuendelea na dodoso kwa Mnyika kesho, huku kesi ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu kutokana na ushahidi unaohusu kauli za viongozi wa CHADEMA, uchaguzi wa mwaka 2025 na madai yanayohusiana na vurugu.

Nzengeli: Na ni kweli mlitoa elimu pale pale kwenye ufunguzi

Mnyika: Ni kweli elimu ilianza kutoka kwenye ufunguzi

Nzengeli: Wewe ni mtaalamu wa sheria au hujui sheria?

Mnyika: Mimi sio mtaalamu wa sheria

Nzengeli: Nitakuwa sahihi nikisema huna utaalamu wowote wa kuchambua hati yoyote ya mshitaka

Mnyika: Ninaweza kuchambua uzoefu wa kutosha wa siasa

Nzengeli :Kama huna sema kama unao sema

Mnyika: Sina

Nzengeli : Kama mtu anauona uchaguzi ni wa haki na uhuru na unageuka kuwa sio wa haki kwa kuwa nyie chadema mmeamua

Mnyika: Akikubaliana na msimamo wetu

Nzengeli: Kama hajakubaliana

Mnyika; Hayo ni maoni yake

Nzengeli: Nimemaliza namualika Job Mrema amalizie waheshimiwa majaji Ahsante

Job : Waambie majaji hii kamusi hii inasemaje hapo juu kwenye kichwa cha habari

Mnyika: Kamusi kuu ya kiswahili Job Toleo la ngapi Mnyika toleo la tatu mwaka 2022

Job : Kwa mujibu wa lichosoma utafiti ulifanywa na nani kuandaa hiyo kamusi

Mnyika : Baraza la kiswahili la taifa

Job: Bakita ndio wamepewa mamlaka ya kufanya utafiti huo

Mnyika: Kwa Tanganyika

Job: Umeulizwa maswali mengi ukawa unasoma kwenye kamusi je ni hiyo uliyoishika hapo toleo la tatu

Mnyiaka: Ndio ndio hii

Job: Unakubaliana mimi kamusi hiyo ndio chombo rasmi cha kutoa tafsiri sahihi ya lugha ya kiswahili

Mnyika: Ni Rasmi ila sio nakala pekee

Job: Mimi sijakuuliza pekee

Mnyika :Hapana

Job: Ni sahihi umeiuizwa kuhusu michango ya tone tone ukasema mmekusanya milioni 302 pesa za Tanzania kuna michango mingine?

Mnyika sina takwimu kamili

Job: Ni kweli kwamba mshaanza kutumia michango ya tone tone na inetumika kiasi gani

Mnyika: Michango hiyo inatumika kwa lengo mahususi na ni michango ya baraza kuu la chama

Job: kama nimekusikia vizuri uliulizwa majukumu yako kama katibu mkuu wa chadema ulishindwa kuyataja ni kweli

Mnyika: hapana sio kweli

Job: Wewe kama mtendaji wa chama una majukumu gani

Mnyika: Msimaizi shughuli zote za kila siku za chama

Job: Kama ndio hivyo ndugu shahidi kama ndio ukweli ni sahihi kwamba umeulizwa maswali mengi ya kiutendaji na unasema hujui

Mnyika: Sio kweli mengi nimejibu ndio isipokuwa machache ambayo ninahitaji uelewa zaidi

Job: Unafikiri ni sahihi chadema kuwa na mtendaji mkuu asiyejua majukumu yake

Mnyika: Ninajua ninachofanya

Job: Nitakuwa sahihi nikesema ukatibu wako mkuu umekuwa wa kusaidiwa saidiwa na ni kama ahsante kwa mwenyekiti wa chadema

Mnyika : Sio sahihi

Job: Je ni sahihi katika utendaji wako umekuwa ukibebwa na mwenyekiti

Mnyika: Hapana

Job: Je ni sahahi hata kizimbani umeshindwa kujieleza mwenyekiti akaja kukunongoneza

Mnyika sio kweli

Job: Ndugu shahidi utakubaliana na mimi kwamba vyama vya siasa vilivyosajiliwa vinatakiwa kufuata sheria za nchi hii kanuni katiba za vyama husika

Mnyika: Ni sahihi Job sasa waambie waheshimiwa majaji nini maana ya fujo ni nini

Mnyika: Fujo ni Fujo

Job; Haya waambie waheshimiwa kwa mujibu wa kamusi uliyo nayo hapo

Mnyika: Bila kuwepo kwa utaratibu mzuri au mpango, hovyo hali ya ghasia na machafuko

Leave a Comment