
CEO wa lebo ya muziki ya The African Princess, mwanamuziki Nandy, amemtambulisha rasmi mwanadada nguli wa muziki wa Bongo Flava, Linah Sanga, kuwa msanii mpya wa lebo hiyo.
Linah sasa anaungana na Pipi Jojo chini ya The African Princess, hatua inayofanya lebo hiyo kuwa na jumla ya wasanii watatu, akiwemo Nandy mwenyewe.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amemkaribisha Linah ndani ya lebo hiyo huku akimuelezea kama “Ndege Mnana” na dada yake mpendwa.

“WELCOME THE AFRICAN PRINCESS LABEL OUR LOVELY SISTER NDEGE MNANA..! @linahafrica,” ameandika Nandy.
Kujiunga kwa Linah kunatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya wasanii wa lebo hiyo, huku The African Princess ikiendelea na dhamira yake ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wasanii wa kike katika muziki wa Afrika.
