×

Watuhumiwa wa Mauaji Wapigwa Risasi na Polisi, Wote Wawili Wafariki Hospitali – Video

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu wawili wanaodaiwa kuhusika katika tukio la ujambazi wa kutumia silaha lililotokea Agosti 29, 2026, eneo la Shewa, Kata ya Mwakibete, Tarafa ya Iyunga jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, tukio hilo lilitokea majira ya saa 5:45 usiku, ambapo Vailenth Libaba (34), mfanyabiashara wa miamala ya fedha, alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Polisi wanasema Vailenth alijeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu watano waliomchoma kwa kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kabla ya kumpora fedha taslimu Shilingi 300,000 pamoja na simu mbili za mkononi zilizokuwa za biashara yake.

Katika ufuatiliaji wa tukio hilo, polisi walifanikiwa kuwakamata watu wawili wanaodaiwa kuhusika. Mmoja ametajwa kwa jina la Venence Yasin, maarufu kama Mnyaki, ambaye kwa mujibu wa taarifa hiyo alitoka gerezani mwaka 2025 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 15 kwa kosa la wizi wa gari.

Mtuhumiwa huyo, polisi wanasema, alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha, lakini aliachiwa huru na Mahakama ya Rufaa baada ya kukata rufaa.

Mtuhumiwa mwingine ni Atupele Kabale, ambaye anadaiwa kuwa na nafasi katika tukio hilo. Polisi wameendelea na mahojiano na upelelezi ili kuwabaini watuhumiwa wengine watatu wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya pia limewataka wananchi wanaomiliki silaha kihalali kuzitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa, huku likitoa wito kwa wananchi wenye taarifa kuhusu watu wanaotumia silaha hizo kufanya uhalifu kuzifikisha polisi.

Aidha, Jeshi hilo limeonya wananchi dhidi ya kutumia silaha kiholela kwa kuwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria na kunaweza kuhatarisha maisha ya watu wengine.

Leave a Comment