
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania, ambapo alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.
Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), na kusababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.
Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, ametangaza mapumziko mafupi ili kuruhusu hali kutulia na hatua zinazohitajika kuchukuliwa.
Hadi sasa, taarifa zaidi kuhusu hali ya kiafya ya Jaji Warioba baada ya kuanguka kwake hazijawekwa wazi.
Mkutano huo ulikuwa ukijadili hali ya kisiasa nchini pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa nchini Tanzania.