×

DStv Yatangaza Ofa Mpya ya ‘Usiwaze’ kwa Wateja

Dar es Salaam, Septemba 7, 2026: MultiChoice Tanzania imetangaza ofa mpya ya “Usiwaze”, inayowawezesha wateja wanaostahili wa DStv kupata kifurushi cha juu zaidi kwa gharama ya kifurushi wanacholipia kwa sasa, bila gharama ya ziada.

Ofa hiyo itaanza Septemba 7 hadi Oktoba 19, 2026, ambapo katika kipindi hicho wateja watakaolipia vifurushi vyao wataweza kufurahia maudhui ya kifurushi kinachofuata juu ya kile walicholipia.

Wateja wapya, waliopo katika huduma na wale ambao huduma zao zilikatika watanufaika na ofa hiyo mara baada ya kulipia vifurushi vyao, na kupata moja kwa moja maudhui ya kifurushi cha juu zaidi bila kuongeza gharama.

Akizungumzia ofa hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Godfrey Bwana, alisema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wateja kufurahia burudani zaidi huku kampuni ikiendelea kuwapatia huduma bora.

“Ofa hii ni kuwathibitishia wateja wetu kuwa tunawathamini na kuwapa fursa ya kufurahia zaidi burudani za kiwango cha aina yake, ikiwemo michezo, filamu, tamthilia, makala maalum, vipindi vya watoto, habari pamoja na maudhui ya ndani,” alisema Bwana.

Kwa mujibu wa MultiChoice Tanzania, ofa hiyo pia itawanufaisha zaidi wapenzi wa michezo, hususan kandanda.

Mteja wa kifurushi cha Shangwe cha Shilingi 40,000, kwa mfano, ataweza kutazama mechi za Ligi Kuu ya England (Premier League) baada ya kulipia kifurushi chake, wakati mteja wa Compact cha Shilingi 68,000 ataweza kufurahia michuano ya UEFA katika kipindi chote cha ofa.

Kwa upande wa wateja wa Compact Plus, watakaolipia kifurushi hicho wataweza kupata maudhui ya kifurushi cha juu zaidi, DStv Premium, katika kipindi cha ofa.

Wapenzi wa tamthilia na maudhui ya ndani nao hawajaachwa nyuma. Wateja wa kifurushi cha Poa cha Shilingi 10,500 watakaolipia huduma zao wataweza kupata chaneli ya Maisha Magic Bongo katika kipindi chote cha ofa.

Baada ya ofa hiyo kumalizika Oktoba 19, 2026, wateja watarudishwa moja kwa moja kwenye vifurushi walivyokuwa wamejisajili na kulipia.

MultiChoice Tanzania imeeleza kuwa ofa hiyo inapatikana kwa wateja wa DStv wanaotumia huduma kwa matumizi ya nyumbani, wakiwemo wateja wapya pamoja na wale wanaorejesha huduma baada ya kukatwa.

Hata hivyo, ofa hiyo haiwahusu wateja wa DStv Premium, DStv Stream, DStv Business, akaunti maalum pamoja na wateja wanaotumia baadhi ya vifurushi vya nyongeza vinavyojitegemea.

Leave a Comment