
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga ‘Chuma’, amefunguka kuhusu sababu ya Bodi hiyo kuwaita wasanii maarufu wa A-List, akiwemo Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Kajala Masanja na Aunty Ezekiel.
Akizungumza kuhusu kikao hicho, Kasiga amesema wito huo ulikuwa na lengo la kufanya marekebisho katika baadhi ya mambo yaliyoonekana kutokuwa sawa katika kipindi cha nyuma, hususan yanayohusiana na masuala ya maadili na weledi katika tasnia ya filamu.
Amesema Bodi inaendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa wadau wa tasnia wanazingatia taratibu, sheria na maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika uzalishaji na uwasilishaji wa kazi za filamu.
Kwa upande wao, wasanii hao maarufu wameeleza kuwa kikao hicho pamoja na uongozi wa Bodi ya Filamu kimekuwa na manufaa, wakisema wamepata fursa ya kuelewa maeneo ambayo walipaswa kuyafanyia maboresho.
Wasanii hao wameahidi kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Bodi, huku wakikiri kuwa wamezitambua baadhi ya makosa yaliyokuwa yakifanyika na kwamba watajitahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha mwenendo na tasnia kwa ujumla.
Kikao hicho kinaonekana kuwa sehemu ya jitihada za Bodi ya Filamu Tanzania katika kuimarisha maadili, weledi na uwajibikaji miongoni mwa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu nchini.
Usikose #Alist kila ijumaa saa 2 usiku chaneli 160 ndani ya Dstv.