
Msanii maarufu wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, ameonekana akiwa na mume wake, Travis Kelce, katika ‘date night’ jijini New York, huku akivutia kwa muonekano wake mpya pamoja na gauni lenye thamani ya takribani TSh milioni 7.2.
Wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 36, walitoka Jumapili, Septemba 6, 2026, na kwenda kupata chakula katika mgahawa maarufu wa Kihindi, Ambassadors Clubhouse New York, uliopo eneo la NoMad, Manhattan.
Swift alivaa gauni refu la hariri lenye mistari kutoka kwa mbunifu Stella McCartney, likiwa na thamani ya takribani dola 2,800 (TSh milioni 7.2). Alikamilisha muonekano huo kwa mkoba wa mbunifu huyo pamoja na viatu vya Aquazzura vya rangi ya metali.

Mbali na gauni hilo, Swift pia alionyesha mtindo wake mpya wa nywele fupi, ambao aliutambulisha Agosti 15, 2026, alipohudhuria harusi ya wahandisi wa muziki, Oli Jacobs na Laura Sisk, nchini Uingereza.
Kwa upande wake, Kelce alivaa shati la mikono mifupi la rangi ya krimu lenye mistari, suruali ya kahawia pamoja na viatu vya rangi nyeusi na nyeupe. Alikamilisha muonekano wake kwa miwani myeusi.
Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza na jarida la PEOPLE, Swift na Kelce walikula katika sehemu ya chini ya mgahawa huo wakiwa pamoja na wanaume wengine wawili. Waliagiza aina mbalimbali za vyakula na vinywaji kutoka kwenye menyu.

WAMEFUNGWA NDOA MIEZI MIWILI ILIYOPITA
Kutoka kwao jijini New York kumekuja takribani miezi miwili baada ya Swift na Kelce kufunga ndoa katika Madison Square Garden Julai 3, 2026.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na takribani wageni 1,000, wakiwemo mastaa mbalimbali na watu mashuhuri kutoka tasnia ya burudani. Sherehe hiyo iliendeshwa na rafiki yao, Adam Sandler.
Wanandoa hao walionekana wakiwa wameshikana mikono walipojitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya ndoa, Julai 10, 2026, katika harusi ya aliyekuwa mchezaji mwenzake Kelce, JuJu Smith-Schuster.
Kumbuka: Thamani ya TSh milioni 7.2 ni makadirio kutokana na dola 2,800 na kiwango cha ubadilishaji kilichotumika kwenye uandishi huu.