Wiki iliyopita niliishia pale yule mama mtu mzima aliyetokea kumpenda Nelly ghafla alipomwuliza Ipyana alikuwa kaenda wapi Nelly akamfahamisha alitoka kidogo. Hakuishia hapo, akamwuliza kama alikuwa akishirikiana naye kuosha magari akamwambia ndiyo. Je, kilifuatia nini? Songa mbele…
“Ila hujaanza kuja hapa muda mrefu eh?” mama huyo katibu muhtasi aliyefiwa na mumewe miaka minne iliyopita alimwuliza Nelly.
“Nimeanza leo,” Nelly alimfahamisha.
“Oke, akija mwenzako nitarudi nataka munioshee gari langu maana leo ni siku ya tano halijaoshwa,” mama huyo alimwambia Nelly.
“Hakuna shida mama yangu,” Nelly alimfahamisha.
Mama huyo alipogeuka na kuanza kuelekea ofisini, Nelly aliyagandisha macho yake kwenye wowowo lake tata lililokuwa likitikisika na kuonekana kama lilitaka kudondoka.
“Kudadeki kumbe huku Posta ndivyo kulivyo? Kila demu mpaka akina mama wote wazuri, asante besti yangu Ipyana kwa kunitoa uswahili, maana hawa wanawake wazuri ningewaona wapi?” Nelly aliwaza.
Mama huyo alipotoweka kabisa, Nelly aliyekuwa na namba za mademu wote aliokutana nao tangu siku ya kwanza kwenda site Madale, aliamua kumpigia demu huyo.
“Haloo! Halooo nani mwenzangu?” yule msichana wa kwanza waliyeachana na Nelly kituo cha daladala Mwenge alimwuliza Nelly baada ya kupokea simu.
Nelly alipojitambulisha, yule dada alifurahi kumsikia na kumwuliza habari za tangu walipoachana, Nelly akamwambia zilikuwa poa kisha alimfahamisha ile ilikuwa namba yake na alikuwa hewani.
Pamoja na yote, Nelly alimwomba dada huyo kama atakuwa na nafasi waonane, akamwambia haikuwa na shida na kupanga Jumapili iliyofuata wakutane Temeke Mwisho.
Alipopewa jibu hilo, Nelly alifurahi sana na kujisemea demu huyo siku hiyo miadi asingechomoa lazima atatafunwa kisawasawa kwani kama ni fedha alikuwanazo.
Baada ya kumalizana na demu huyo, alimwendea hewani Atu ambaye tangu walipoachana siku ile walipobilingishana katika gesti ya Keko hawakukutana.
Msichana huyo ambaye hakuwa na namba ya Nelly alipomwuliza alikuwa nani, sharobaro Nelly akajitambulisha, Atu alifurahi na kumwambia kwa nini alikuwa kimya namna ile!
“Jamani si nilikwambia simu yangu iliibiwa, hiyo ndiyo namba yangu halafu nahamu mno ya kukutana na wewe,” Nelly aliyeamua kuwashughulikia vilivyo viumbe hao alimwambia.
“Ni wewe tu! Mimi hata ukisema leo nipo tayari!” Atu alimwambia Nelly.
Kitendo cha msichana huyo kumwambia Nelly hata siku ile alikuwa na chansi, kijana huyo mpenda mademu wazuri akaona atafanya kosa kubwa sana kumuachia ndege huyo aliyeingia tunduni mwenyewe.
“Oke! Mimi kwa sasa nipo tauni, nikimaliza mambo ya hapa nitakupigia na kukuelekeza sehemu ya kumiti, au iwe pa siku ile?” Nelly alimwambia Atu aliyesema sawa.
Wakati Nelly akiendelea kuzungumza na Atu, Ipyana alirudi ndipo akamuaga Atu na kumfahamisha kuhusu yule mama mtu mzima aliyejaaliwa bambataa matata.
“Umesema mnene mfupi, kajazia nyuma?” Ipyana alimwuliza Nelly.
“Yeah! Tena akitembea utafikiri mzigo unataka kuanguka wenyewe yaani kaka wanawake wa hapa wazee kwa vijana wote moto kwa kwenda mbele,” Nelly alimwambia Ipyana.
“Mimi naangalia kazi tu, kama ningewaendekeza nisingekuwa nimefanya chochote, hivi unajua kama nimenunua uwanja nataka mwakani nianze kujenga?” Ipyana alimwambia Nelly.
Nelly alipoambiwa hivyo alicheka sana na kumwambia kweli hakuutendea haki ujana, badala ya kufurahia maisha eti anafikiria kujenga wakati mshua wake ana nyumba tatu kali na mbili kapangisha.
“Zile ni za mshua mimi nataka niwe na nyumba yangu,” Ipyana alimwambia Nelly aliyeishia kucheka.
“Ndiyo hivyo, baada ya kumwambia haupo akaniuliza maswali mawili matatu akaniaga na kusema atarudi ukija ngoja tumsubiri,” Nelly akamwambia Ipyana.
“Huyo mama anaitwa mama Maduu alifiwaga na mumewe kitambo tu na siyo bahili wa fedha zake,kwani kuna wakati nikimuoshea gari lake hunipa mpaka shilingi elfu kumi,” Ipyana alimwambia rafiki yake.
Je, kilifuatia nini? Usikose wiki ijayo. Maoni tumia namba hiyo hapo juu.