
Vodacom Tanzania Foundation imetoa madawati kwa Shule ya Msingi Makumbusho, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule mbalimbali kupitia msafara wa Nyerere Cycling Tour 2026.
Katika hafla hiyo, Afisa Miradi ya Jamii wa Vodacom Tanzania Foundation, Deborah Kaluzi (kulia), alimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Yasini Shehaghilo (kushoto), moja ya madawati yaliyotolewa.
Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Archie James Killo (wa pili kushoto), pamoja na Mwanzilishi wa Nyerere Cycling Tour, Gabriel Landa (wa pili kulia).
Mpango huo unalenga kuboresha miundombinu ya elimu na kuchochea maendeleo ya jamii zilizopo kando ya njia ya msafara huo kupitia ujenzi na ukarabati wa madarasa, utoaji wa madawati na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ya jamii.