
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika taasisi za umma, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, Oktoba 13, 2026.
Katika uteuzi huo, Dkt. Thereza Israel Mugobi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mugobi alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Aidha, Bw. Said Rajabu Mndeme ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mndeme alikuwa Mkurugenzi wa Milki katika Wakala wa Majengo Tanzania.
Uteuzi huo umetangazwa na Shaaban Kissu, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Dar es Salaam.
