Vodacom Nyerere Cycling Tour Yaweka Alama ya Maendeleo Kwa Jamii Kuenzi Fikra za Baba wa Taifa
Hashpower7113 October 14, 2026 408 views 0 Comments
SHARE THIS:
Waendesha baiskeli walioshiriki Nyerere Cycling Tour 2026 wakiwa nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara, wakati wa kuhitimisha msafara huo uliohusisha zaidi ya waendesha baiskeli 200 na kufadhiliwa na Vodacom Tanzania.
Mbali ya kuenzi fikra na falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kupitia michezo, mashindano ya baiskeli ya Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026 yameendelea kuacha alama ya maendeleo kwa jamii.
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Madaraka Nyerere (katikati), akizungumza na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kushoto) na Mkurugenzi wa Tehama wa kampuni hiyo, Athumani Mlinga, wakati wa hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere iliyofanyika Mwitongo, Butiama mkoani Mara. Tukio hilo ni sehemu ya Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc, ili kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere kupitia michezo na miradi ya maendeleo ya jamii.
Hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere iliyofanyika nyumbani kwake Mwitongo, Butiama mkoani Mara, imebeba ujumbe wa kuunga mkono miradi ya kijamii kama sehemu ya urithi wa fikra zake.
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Vodacom Tanzania PLC na Stanbic Bank Tanzania wakati wa kilele cha msafara wa Baiskeli wa Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026 zilizofikia tamati Butiama, mkoani Mara leo. Hafla hiyo ni sehemu ya Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc, ili kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere kupitia michezo na miradi ya maendeleo ya jamii.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc, yanatumika kama jukwaa la kuhamasisha mshikamano, afya na maendeleo ya jamii.
Waendesha baiskeli wakiingia nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara, wakati wa kuhitimisha msafara wa Vodacom Nyerere Cycling Tour 2026, msafara huo umedhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc na kushirikisha zaidi ya waendesha baiskeli 200.Waendesha baiskeli walioshiriki Nyerere Cycling Tour 2026 wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc katika kijiji cha Mwitongo, Butiama, mkoani Mara, baada ya kuhitimisha msafara wa kilomita 1,450 kutoka Bagamoyo, uliofanyika kwa lengo la kuenzi urithi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ukihamasisha maendeleo ya jamii kupitia michezo.