×

Mahakama Yakataa Maombi ya Kuizuia Chadema Kufanya Shughuli za Kisiasa

Maombi ya kutaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kizuiwe kufanya shughuli za kisiasa nchini yamekataliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo chama hicho kitaendelea na shughuli zake za kisiasa kama kawaida.

Katika uamuzi uliotolewa leo, Oktoba 22, 2026, na Jaji Awamu Mbagwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Mahakama imesema haioni sababu za msingi za kukizuia chama hicho kuendelea na shughuli zake za kisiasa.

Leave a Comment