×

Tpsf, Tantrade Wakutana na Mfanyabiashara Gachuma Mwanza

Mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa CMG Group, Christopher Gachuma, amekutana na Wakurugenzi wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)Bw. Deogratius Massawe na Wakala wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bw. Ephraim Mafuru jijini Mwanza
Mkutano huo ulilenga kuimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za umma, kukuza fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, Gachuma amepongeza juhudi za TPSF na TANTRADE za kushirikiana katika kukuza biashara, kuunganisha wadau na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.
Aidha, Mkurugenzi wa MWATEX aliyeshiriki katika kikao hicho pia amepongeza juhudi za taasisi hizo mbili, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu katika kuendeleza biashara na uwekezaji nchini

Leave a Comment