Vodacom Tanzania yaendelea kukuza Golf nchini, Paul Chidale aibuka kinara Vodacom Tanzania Open 2026
Hashpower7113 October 25, 2026 96 views 0 Comments
SHARE THIS:
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mshindi kutoka Malawi Paul Chidale, tuzo baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha, Chidale alimaliza mashindano hayo kwa mikwaju 289 na kujinyakulia Sh9.35 milioni, akifuatiwa na Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza wa tatu kwa mikwaju 294.
Mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yamehitimishwa jijini Arusha kwa mafanikio makubwa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni ya Vodacom Tanzania kuendelea kukuza na kuinua mchezo wa Golf nchini.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Katika mashindano hayo, mchezaji kutoka Malawi, Paul Chidale, aliibuka mshindi na kujinyakulia Sh9.35 milioni baada ya kumaliza kwa mikwaju 289, akiwashinda Nuru Mollel wa Tanzania na Robinson Owiti wa Kenya.
Katika mashindano hayo yenye ushindani mkali, mchezaji kutoka nchini Malawi aliibuka bingwa baada ya kumaliza raundi zote kwa jumla ya mikwaju 289.
Mshindi huyo alijinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 9.35 kama zawadi ya ushindi.
Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mchezaji golf kutoka Malawi, Paul Chidale, mfano wa hundi ya Sh9.35 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha. Chidale alimaliza mashindano hayo ya siku nne kwa jumla ya mikwaju 289, akimzidi Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza nafasi ya tatu kwa mikwaju 294.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na mchezaji Mtanzania aliyemaliza kwa mikwaju 293, huku nafasi ya tatu ikienda kwa mchezaji kutoka Kenya aliyehitimisha mashindano kwa mikwaju 294.
Tuzo kwa washindi zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa kitengo cha biashara wa kampuni hiyo mdhamini.
Baadhi ya washiriki na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye mazoezi wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha. Mashindano hayo ya siku nne yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine mbalimbali, wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.Rais wa chama cha Golf nchini (Tanzania Golf Union – TGU) Gilman Kasiga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Vodacom Tanzania Open katika kukuza ushindani na kuendeleza mchezo wa golf nchini, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Kili Golf Course jijini Arusha, Oktoba 22 hadi 25, 2026. Mashindano hayo yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi mbalimbali wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.