
Askari wa Kikosi cha Polisi Reli wamefanya doria maalumu ya kiusalama katika eneo la Malindi, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya reli.
Doria hiyo imeongozwa na Sajenti wa Polisi Rahabu Mbaruku, akishirikiana na Koplo wa Polisi Said Ally, ambapo wametumia mbwa maalumu wa Polisi waliofunzwa kubaini silaha na vilipuzi.
Matumizi ya mbwa hao ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha ulinzi katika maeneo ya miundombinu ya reli, kubaini viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama na kuzuia vitendo vya uhalifu.

Kupitia doria hiyo, Kikosi cha Polisi Reli kinaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha maeneo ya reli yanakuwa salama kwa shughuli za usafirishaji na matumizi mengine yanayohusiana na miundombinu hiyo.
Wananchi pia wanahimizwa kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu vinavyoweza kuhatarisha usalama wa miundombinu ya reli.


