×

MUHAS Yatangaza Nafasi 10 za Kazi, Waombaji Watakiwa Kuwa na GPA ya 3.8

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetangaza nafasi 10 za ajira za Tutorial Assistant katika kada mbalimbali za afya na sayansi, kikitoa fursa kwa wahitimu wenye sifa kuomba nafasi hizo.

Tangazo hilo lililotolewa Novemba 15, 2026, linaeleza kuwa ajira hizo zinalenga kuongeza idadi ya watumishi watakaosaidia kufundisha programu mbalimbali katika shule saba na taasisi moja ya kitaaluma za chuo hicho. Soma zaidi >>NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI (MUHAS)

Nafasi za kazi zilizotangazwa

Kwa mujibu wa tangazo hilo, nafasi hizo ni:

  1. Tutorial Assistant – Haematology and Blood Transfusion (nafasi 1).

  2. Tutorial Assistant – Radiation Therapy (nafasi 1).

  3. Tutorial Assistant – Parasitology and Medical Entomology (nafasi 1).

  4. Tutorial Assistant – Environmental Health (nafasi 1).

  5. Tutorial Assistant – Psychology (nafasi 1).

  6. Tutorial Assistant – Human Nutrition (nafasi 1).

  7. Tutorial Assistant – Internal Medicine (nafasi 1).

  8. Tutorial Assistant – Surgery (nafasi 1).

  9. Tutorial Assistant – Paediatrics and Child Health (nafasi 1).

  10. Tutorial Assistant – Obstetrics and Gynaecology (nafasi 1).

Sifa za waombaji

MUHAS imeeleza kuwa waombaji wanapaswa kuwa na shahada zinazohusiana na kada husika kutoka chuo kikuu kinachotambulika, huku kigezo muhimu kikiwa ni kuwa na wastani wa alama (GPA) usiopungua 3.8 kati ya 5.0.

Kwa nafasi za Internal Medicine, Surgery, Paediatrics and Child Health pamoja na Obstetrics and Gynaecology, waombaji wanatakiwa kuwa na shahada ya Doctor of Medicine au sifa za Bachelor of Medicine and Bachelor of Surgery (MBBS).

Aidha, waombaji wote wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania na wasiozidi umri wa miaka 45, isipokuwa wale ambao tayari wako katika Utumishi wa Umma.

Nyaraka zinazohitajika

Waombaji wanapaswa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:

  • Wasifu binafsi (CV) wenye mawasiliano sahihi.

  • Nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na transcript.

  • Vyeti vya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita.

  • Vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika.

  • Cheti cha kuzaliwa.

  • Picha ya hivi karibuni ya passport size kwenye mfumo wa maombi.

  • Majina na mawasiliano ya wadhamini watatu (referees).

Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na kuelekezwa kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala (DVC-PFA), MUHAS.

Jinsi ya kutuma maombi

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pekee.

Tovuti ya maombi:

Tarehe ya mwisho: 22 Novemba 2026

MUHAS imesisitiza kuwa waombaji watakaofaulu hatua ya awali ya uchambuzi wa maombi pekee ndio watakaowasiliana kuhusu tarehe ya usaili.

Aidha, chuo hicho kimeonya kuwa matumizi ya vyeti vya kughushi au kutoa taarifa zisizo sahihi yanaweza kusababisha hatua za kisheria.

Kwa wahitimu wenye sifa zinazotakiwa, hii ni fursa ya kujiunga na taasisi ya elimu ya juu inayojihusisha na mafunzo ya wataalamu wa afya nchini Tanzania.

Leave a Comment