×

Singida Black Stars Yaichapa Azam Fc 4-2 Uwanja Wao wa Nyumbani

Singida Black Stars wameandika ushindi muhimu wa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Azam FC walianza vizuri kwa kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1, kupitia Feisal Salum aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 27 na Zidane aliyeongeza bao la pili dakika ya 29.

Kwa upande wa Singida Black Stars, Keyekeh aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 40 na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa tofauti ya bao moja.

Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kabisa baada ya Singida Black Stars kurejea kwa kasi na kuonyesha makali makubwa ya ushambuliaji. Mwashinga alisawazisha dakika ya 52 kabla ya Sowah kuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Azam FC kwa kufunga mabao mawili dakika ya 68 na 73.

Mabao hayo yaliihakikishia Singida Black Stars ushindi wa 4-2, huku Azam FC wakikosa nafasi ya kulinda faida ya mabao waliyokuwa nayo kipindi cha kwanza licha ya kucheza nyumbani.

Matokeo hayo yanaipa Singida Black Stars pointi tatu muhimu katika mbio za Ligi Kuu ya NBC, huku Azam FC wakilazimika kujipanga upya baada ya kupoteza mchezo huo mbele ya mashabiki wao.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Namungo FC na Mbeya City zilitoka sare ya bila kufungana (0-0).

Leave a Comment