×

Rais Samia Ethiopia, Watoto wa Kitanzania Wampa Mapokezi Maalum

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Ethiopia waliojitokeza kumlaki baada ya kuwasili nchini humo tarehe 22 Novemba, 2026 kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili. Akiwa Addis Ababa, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), pamoja na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyowasili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, Novemba 22, 2026, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Baada ya kuwasili nchini humo, Rais Samia alipokelewa na Watoto wa Kitanzania wanaoishi Ethiopia waliojitokeza kumlaki na kuonesha furaha yao ya kukutana na kiongozi huyo wa nchi.

Akiwa nchini Ethiopia, Rais Samia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), unaowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kujadili masuala ya afya ya umma barani Afrika.

Katika ziara hiyo, Rais Samia pia anatarajiwa kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, hatua inayolenga kuimarisha juhudi za kuboresha huduma za afya kwa wanawake na watoto katika mataifa ya Afrika.

Ziara hiyo ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa yanayolenga kujadili changamoto za afya na kuimarisha ushirikiano wa maendeleo barani Afrika.

Leave a Comment