×

Jini Mauti-28

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Nililetewa bakuli kubwa lililojaa nyama nyingi, nilipoletewa, nikaliweka juu ya meza na kuanza kuchukua kipande kimoja baada ya kingine.
SASA ENDELEA…

Hapa naomba niwaambie kitu, unapokuwa katika uwanja wa wachawi na kuletewa nyama za watu, usifikiri kwamba utaiona chungu au kugundua mara moja kwamba nyama unayokula si ya mnyama, kwako itakuwa tamu kama unakula nyama ya ng’ombe.
Nilikula sana nyama huku wachawi wengine wakinifuata na kunipongeza, kazi niliyoifanya ya kumpeleka Michael pale uwanjani ilikuwa kubwa na ilinijengea heshima zaidi. Michael na watu wengine niliowaua walikuwa ndani ya banda moja kubwa ambalo ndilo tulilohifadhia misukule mingine.

Kila wakati nilikwenda kule na kuwaangalia, hawakuwa wakinifahamu, waliniona lakini kwao nilionekana mgeni kabisa. Wanaume niliowapenda sana walikuwa ndani ya chumba kimoja, nilipowaangalia nilijisikia vibaya ila sikuwa na jinsi, ilitakiwa iwe kama ilivyokuwa.

Siku hiyo tulitakiwa kuondoka mapema uwanjani hapo kwa kuwa kesho yake tulikuwa na mkutano mkubwa wa kitaifa hivyo tulihitajika kujiandaa.
Asubuhi ilipofika, nilikwenda shuleni. Kwa mbali nilianza kusikia vilio, sikutaka kujiuliza kwamba nini kiliendelea, nilijua fika kwamba taarifa za msiba wa Michael zilisambazwa shuleni hapo.
Moyo wangu uliumia mno, nikajikuta nikibubujikwa na machozi mashavuni mwangu, niliumia kwa kile kilichotokea. Wanafunzi walibembelezana tu, nikajifanya sijui kilichotokea, nilichofanya ni kuwasogelea baadhi ya wanafunzi na kuwauliza.

“Michael amekufa, alikutana na jini jana usiku kule Coco Beach,” aliniambia mwanafunzi mmoja, uso wake ulikuwa na majonzi tele.
“Michael amekufa?” nilijifanya kuuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo! Jini amemuua,” aliniambia mwanafunzi mwingine.
Hawakujua nilijisikiaje, niliumia moyoni mwangu lakini sikuwa na jinsi. Siku hiyo shuleni hapo hata walimu hawakufundisha, walibaki ofisini mwao tu. Mchana ulipofika ndipo tetesi zikaanza kusambaa kwamba jinsi Michael alivyokufa, kifo cha aina ileile ndicho alichokufa Hemedi wiki chache zilizopita.
“Kwa hiyo jini aliyemuua dereva bodaboda ndiye aliyemuua Michael?” alihoji mwanafunzi mmoja.
Wanafunzi tukajiandaa na kuelekea msibani. Hatukuwa wanafunzi wengi ila tulichaguliwa baadhi. Wakati tukiwa njiani ndipo nilipogundua kitu. Sifael, mvulana aliyenipenda sana ambaye mara kwa mara alikuwa akiniangalia, alionekana kubadilika.

Aliniangalia kwa macho yaliyojaa hofu, alionekana kama mtu aliyeniogopa mno. Sikujua kitu gani kiliendelea, nikajifanya kutokujali, niliendelea na safari. Tulipofika msibani, tukawapa pole wafiwa na baada ya dakika chache, Sifael akaniita, japokuwa aliniogopa, siku hiyo alionekana tofauti.
“Unajua ukweli,” aliniambia.
“Ukweli upi?”
“Juu ya kifo cha Michael.”
“Hapana! Sijui chochote.”
“Davina, utakuwa unajua tu ukweli. Kama hukumuona huyo jini, basi wewe ndiye jini mwenyewe,” aliniambia Sifael.
“Mimi jini?”
“Ndiyo! Jana usiku nilikuona unaondoka na Michael kuelekea kule kwenye miamba, tena kulikuwa na giza,” aliniambia Sifael, nikashtuka japokuwa sikutaka kumuonesha mshtuko wangu.
“Mimi?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Utakuwa umenifananisha.”
“Yaani mimi nikufananishe wewe?”
“Inawezekana!”
“Haiwezekani! Ni wewe. Davina, umemuua Michael,” aliniambia huku akionekana kuanza kuogopa.
“Nimemuua Michael?”
“Ndiyo.”
Sifael hakutaka kuzungumza sana, kila aliponiangalia, alizidi kuwa na hofu.

Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wake wiki ijayo.

Nahisi aliona akiwa amesimama na mtu asiyekuwa wa kawaida hata kidogo, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo huku akionekana kuchanganyikiwa.
Alikwenda katika kundi la wanafunzi na kutulia katikati, alionekana kuogopa sana, kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Niliingiwa na wasiwasi kwa kuona kwamba kama nisingefanya jambo fulani basi Sifael angeweza kuwaambia watu wengine kwamba jana aliniona nikiondoka na Michael kwenda kule kwenye miamba.
Nilichokifanya ni kuondoka kuelekea chooni, huku, nilisimama na kisha kuanza kuzungumza maneno ya kichawi, hapohapo nikapotea na kutoka chooni. Hakukuwa na mtu aliyeniona, nilikuwa nikitembea kuelekea kule kulipokuwa na kundi la wanafunzi ambapo Sifael alikuwa mmojawao.
Nilipofika, nikamnyooshea kidole, hapohapo akadondoka chini. Hakukuwa na mtu aliyeniona, walimuona Sifael akidondoka peke yake tu. Pale chini alipokuwa, akaanza kukakamaa mwili, wanafunzi wakakimbia, wazee wakakusanyika kumwangalia, hawakujua nini kiliendelea, mapovu yakaanza kumtoka.
Nilifanya hivi kwa kuwa sikutaka Sifael atoe siri ya kile kilichotokea jana. Hapo nikarudi chooni ambapo nilijitoa kwenye hali ya kichawi na kuwa kawaida. Nikatoka chooni na kuelekea kule watu walipomzunguka Sifael.

*****
Kuanzia siku hiyo sikutaka kujihusisha na wanaume, niliogopa kwa kuwa nilijua kwamba endapo ningefanya mapenzi na mwanaume yeyote yule ilikuwa ni lazima afe kama ilivyotokea kwa wengine.
Katika kipindi chote hicho mama hakuwa amejua kwamba nilikuwa mchawi, sikuonyesha dalili zozote zile, nilikuwa mkimya na mpole. Wanaume wengine walikuwa wakinifuata nyumbani, wengi walinitongoza lakini msimamo wangu ulikuwa uleule kwamba sikuhitaji mwanaume yeyote yule.
Nilisoma mpaka kidato cha nne na matokeo yalipotoka, nilifanya vizuri na hivyo kwenda kujiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamini iliyokuwa jijini Dar .
Hapo shuleni nikamuona mvulana mmoja, mvulana mwenye sura nzuri ambaye kwa kumwangalia, kuna kitu nilichohisi kwamba hakuwa sawa, Nitakueleza kwa nini hapo baadaye.
Mvulana huyu aliitwa John. Alikuwa kidato cha tano, hakuwa muongeaji sana, maisha yake yalitawaliwa na upole

Leave a Comment