
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa.
MBUNGE wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 30 akiwa kwenye Kamati za Bunge.
Ndasaa anakuwa mbunge wa nne wa CCM kupandishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa baada jana wabunge Mh.Kangi Lugola wa jimbo la Mwibala, Mh.Sadiq Murad wa jimbo la Mvomero na Mh.Victor Mwambalaswa wa jimbo la Lupa kupandishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30 toka kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Gairo ili taarifa yake ipitishwe bila kujadiliwa.