
Luis Suarez kulia akishangilia bao lake la kwanza kwenye mechi ya jana zidi ya Atletico Madrid.
Torres baada ya kuifungia Atletico bao kwenye mechi ya jana usiku zidi ya Barca.
Atletico wakishangilia.
Torres akipigwa kadi nyekundu.
Lionel Messi akiwazua.
Suarez akishangilia bao lake la pili.
Messi na Suarez wakipongezana.
Luis Suarez aliipa ushindi klabu yake ya Barcelona kwenye Champions League baada kuifunga Atletico Madridbao 2-1, Nou Camp.
Fernando Torres ndiye alianza kuifungia Atletico kunako dakika ya 25 kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi wanakwenda mapumzikoni. Kipindi cha pili Suarez alisawazisha na baadaye kuongeza bao la pili na la ushindi kwa Barca.