×

Ronaldo apiga hat trick, Man City yaifumua PSG

331C781700000578-3536415-image-a-40_1460491059347

Cristiano Ronaldo akishangilia goli aliloipatia timu yake katika mchezo uliopigwa jana, na kufanikiwa kuifungia ‘hat-trick’.

331CB4B600000578-3536415-Cristiano_Ronaldo_passionately_celebrates_after_scoring_a_hat_tr-m-27_1460507057092

….Akishangilia baada ya kufunga goli la pili katika mtanange huo.

331CB60E00000578-3536415-image-a-1_1460492856286

….Akipiga shuti kali lililomshinda kipa wa Wolfsburg na kufanikiwa kutinga kimiani na kufanya karamu hiyo ya magoli kufikia 3-0.

331CB34A00000578-3536466-image-a-69_1460492837569

Kevin De Bruyne akiifungia timu yake goli muhimu katika mchezo dhidi ya PSG, na kuifanya Man City kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

331CB99200000578-3536466-image-a-75_1460493079441

De Bruyne (kulia) akishangilia goli hilo pamoja na mchezaji mwenzake Fernandinho.

331C135200000578-3536466-image-m-43_1460488125482

Straika wa Man City Sergio Aguero akijaribu kuwatoka wachezaji wa PSG.

Madrid, Hispania
REAL Madrid usiku wa kuamkia leo walifanikiwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku PSG wakitupwa nje na Manchester City.

Katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid walikuwa wanapewa nafasi ndogo ya kufuzu kwa hatua hiyo baada ya mchezo wa kwanza kuchapwa mabao 2-0 na Wolfsburg ya nchini Ujerumani.

Hata hivyo, vijana hao walio chini ya kocha Zinedine zidane, waliingia uwanjani wakiwa na nguvu kubwa na kufanikiwa kujipatia mabao mawili ndani ya dakika mbili tu.

Staa wa timu hiyo Cristiano Ronaldo aliendelea kuonyesha maajabu yake baada ya kufunga bao la kwanza katika dakika ya 16 kutokana na kuiwahi krosi iliyopita na Dani Carvajal katikati ya mabeki wa Wolfsburg na kumkuta mfungaji.

Hata hivyo, ilimchukua Ronaldo dakika moja tu kupachika bao la pili kwa kichwa safi kutokana na kona safi iliyopigwa na Carvajal ambaye alionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo.

Mabao hayo yaliwafanya mashabiki wa Santiago Bernabeu wachanganyikiwa kwa kuwa matokeo yalikuwa 2-2, lakini iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 77, kujipatia bao la tatu lilowekwa kimiani tena na Ronaldo na kujihakikishia nafasi ya nusu fainali huku akipiga hat trick yake kwenye mchezo huo.

Man City vs PSG

Mchezo mwingine mkali ulipigwa kwenye Uwanja wa Etihad huku timu mbili za Manchester City na PSG zikitafuta kwa mara ya kwanza nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Ufaransa, PSG walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na walijua kabisa kuwa lazima wapate ushindi nchini England au sare ya zaidi ya mabao 3-3 ndiyo inaweza kuwavusha.

Hata hivyo, huku dakika zikiyoyoma, Manchester City waliamka kipindi cha pili na kufanikiwa kujipatia bao safi kupitia kwa Kevin de Bruyne katika dakika ya 73 na kuwapa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 na kuwapeleka kwenye hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza.

Leave a Comment