×

Tamfi, Citi Bank zazindua tuzo kwa wajasiriamali wadogo

1.Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa taasisi ya kifedha (TAMFI), Winnie E.Terry,Mkurugenzi Mkuu wa Citi Bank, Joseph Carasso na Ofisa Mahusiano wa ,Frank Kallaghe.Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kifedha (TAMFI), Winnie E.Terry, Mkurugenzi Mkuu wa Citi Bank, Joseph Carasso na Ofisa Mahusiano wa Citi, Frank Kallaghe.

2.Katibu Mtendaji wa taasisi ya kifedha (TAMFI), Winnie E. Terry (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo.Katibu Mtendaji wa Tamfi, Winnie E. Terry (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo.

3.Hafla hiyo ikiendelea.Hafla hiyo ikiendelea.
4.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

  MTANDAO wa Asasi za Huduma za Kifedha ujulikanao kama ‘TAMFI’ kwa kushirikiana na Citi Bank, leo Alhamisi umezindua mkakati wao wa Tuzo za Citi 2016 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wanaofanya biashara ndogondogo hapa nchini.
Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Citi Bank jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Citi Bank, Joseph Carasso, alisema kuwa kama sehemu ya mwendelezo wa Citi kwenye eneo la mikopo midogo midogo wanayofuraha kuwatangazia nia yao ya mkakati wa kuendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo kwa kupitia utoaji tuzo za Citi kwa kila mwaka huku akisema hasa watazingatia mafanikio ya baadhi ya wajasiriamali wenye ubunifu hapa Tanzania.

Alisema mkakati huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa kutambua michango ya wajasiriamali wadogo na pia michango ya asasi zinazotoa huduma za kifedha kwenye maeneo yao ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 14.5 tayari zimewekezwa kupitia asasi za Huduma za Kifedha (Microfinance Networks) na Asasi za Kifedha (MFLs) ili kujumuisha wadau muhimu ambao watashawishi miundombinu ya sera na kanuni zinazoruhusu ubunifu duniani kote.

Aidha, Carasso alisema mkakati huo unafanyika kwenye nchi 30 ikiwemo Tanzania ambapo zaidi ya maelfu ya wajasiriamali wanaofanya kazi kwa bidii walichaguliwa na taasisi za kifedha na mamia kati yao walipata zawadi na kupunguza umaskini.

Alieleza mchakato wa upatikanaji wa wajasiriamali hao utafanyika kupitia taarifa zao za kibiashara kupitia wataalamu wa Huduma za Mikopo (Microfinance) ili kuweza kuwapata washindi ambapo taarifa zao zitajadiliwa na wataalamu wanaotoka kwenye sekta binafsi, umma na wanazuoni ambapo mashindano hayo yataendelea hadi Juni, mwaka huu.

Naye Katibu Mtendaji wa Tamfi, Winnie E.Terry, alisema fursa zitatolewa kufuatana na idadi ya watu, kanda, jinsia na shughuli za kiuchumi ambapo vigezo vya ushindi vitalenga biashara inavyokua, faida, ubunifu na fursa za ajira.
“Biashara husika iwe imebadilisha maisha ya mjasiriamali husika ikiwemo familia yake na jamii inayomzunguka. Kwa atakayehitaji kupata ufafanuzi zaidi awasiliane nasi kwa namba hizi, +255 764 668 331au +255 222 211 226,” alisema Terry.

Stori: Denis Mtima na Imelda Mtema/Gpl

Leave a Comment