×

Usiku wa Uswazi Dar Live, Msagasumu, Nature na Snura, Kukinukisha

JUMA nJuma Nature

Gabriel Ng’osha

WAKALI wa Muziki wa Mchiriku, Mduara na mwingineo, Snura Mushi ‘Snura’ Msagasumu na Juma Nature, Aprili 23, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar watakinukisha katika shoo kali ya Usiku wa Uswazi.

msagasumu akiimba wimbo wa shemeji unanitega (2)

Msagasumu

Akizungumza na mwandishi wetu, mratibu wa shoo hiyo, Ester Kiama alisema Usiku wa Uswazi ni maalum kwa ajili ya muziki wa asili ya Tanzania ambapo mashabiki watapata kuona ladha ya muziki huo kwa kiingilio cha Shilingi 7,000 sambamba na burudani ya kukata na shoka.

snura dua (3)Snura Mushi ‘Snura’

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuunga mkono tamasha la Usiku wa Uswazi kwani kila mwaka litakuwa linafanyika ili kuupa thamani muziki wa asili ya Kitanzania huku mastaa kibao kutoka Bongo Muvi wakiongozwa na Gabo Zigamba nao watakuwepo,” alisema Ester.

Leave a Comment