
Rais Dk. Magufuli.
RAIS Dk. John Pombe Magufuli amewasili katika daraja la kisasa la Kigamboni tayari kwa uzinduzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 680.
Daraja hilo lililogharimu shilingi bilioni 214.6 linaunganisha eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za wakandarasi wa mradi huo, Daraja hilo litakuwa na barabara sita, tatu kila upande, na pia njia za waenda kwa miguu (Pedestrians).

Hali pametengwa milango kwa ajili ya matumizi ya magari aina tofauti.
Geti namba 1 ni kwa wale wenye vibali maalum, geti namba 2 geti namba 3 na geti namba 4 ni wenye magari madogo binafsi, geti namba 5 ni mini bus (daladala) na Geti namba 6 nimaalum kwa malori.
Daraja hilo ambalo ujenzi wake umeanza Februari 1, 2012 ni mradi wa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 40 na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF yenye asilimia 60.