Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Na Waandishi Wetu, Ijumaa
Dar es Salaam: MAHABA niue! Hiyo ndiyo kauli nzuri unayoweza kuitumia kuelezea uhusiano wa kimapenzi unaoendelea kati ya staa wa Ngoma ya Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na ‘video queen’ anayekuja kwa kasi, Lulu Abbasi ‘Lulu Ladiva’.
Madai ya kwamba wawili hao ni wapenzi, yaliwasilishwa kwenye dawati la gazeti hili na chanzo chetu ili kupata ukweli, Ijumaa liliingia mzigoni.
Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Lulu Ladiva ambapo alikiri kuwa in love na mwanamuziki huyo, akafunguka:
“Kweli kabisa nipo ‘in love’ na Nay wa Mitego, tena sasa ni muda mrefu tumekuwa wote sema mwanzo hatukupenda kuweka penzi letu hadharani, najivunia kuwa na Nay kwa kuwa ananiheshimu na kunijali japo migongano kwenye uhusiano huwa haikosi, mimi nipo tayari kumvumilia kwa namna yoyote ile kwani moyo wangu umeshapenda na sioni kitu cha kututenganisha tena.”
Kwa upande wake Nay alisema: “Lulu Ladiva kwa sasa ndiye usingizi wangu sema mmechelewa kujua, mbona kitambo tu nipo naye maana tangu nimeachana na Shamsa huyu ndiye demu aliyeshikilia mikoba yake.”
KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA IJUMAA, LEO April 22, 2016
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz
