Kanye West na mkewe Kim Kardashian.
DIVA anayekinukisha mbaya kwenye anga la wanamitindo ughaibuni, Kim Kardashian amedai kuwa mumewe Kanye West anahitaji mtoto wa tatu haraka iwezekanavyo ingawa ni muda mchache tu umepita tangu wawili hao wapate mtoto wao wa pili aitwaye Saint West.
Kim aliyasema hayo hivi karibuni huku akiongeza kuwa ingawa yeye hajawa tayari kupata mtoto mwingine kutokana na ukweli kuwa wanawe North na Saint bado ni wadogo lakini huenda matakwa ya mumewe yatamzidi nguvu.