×

Zawadi ya gari kwa Blac Chyna Yazua Kizaazaa

rob-kardashian-blac-chyna-birthday

Rob Kardashian na Blac Chyna

ZAWADI ya gari jipya aina ya Lamborghini lenye rangi ya pinki ambayo kaka wa mwanamitindo Kim Kardashian, Rob Kardashian amempa mchumba wake Blac Chyna limezua kizaazaa ndani ya familia yake baada ya dada zake Rob kudai Blac anamfanyia mchezo mbaya kaka yao.

Dada hao ni Khloe Kardashian na Kylie Jenner ambao wamesema kutokana na wifi yao huyo kuwahi kufanya kazi kasino akicheza uchi huenda anatabia mbaya zenye ushawishi wa kufaidika zaidi kupitia uhusiano ambazo ndizo anamfanyia kaka yao mpaka anakuwa anampa mara kwa mara zawadi kubwa. Hata hivyo, kuna habari nyepesinyepesi zinadai Blac na dada wa Rob hawana uhusiano mzuri!

Leave a Comment