Sabrina Gharib (19) anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo kwenye Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, leo ametembelea Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online.
Sabrina Gharib (kulia) akiwa na mama yake Asha Ramadhani wakiendelea kufanya mahojiano.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka akiongea nao jambo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global wakizungumza jambo na wageni hao.
Sabrina Gharib akiwa katika mapozi tofauti na wafanyakazi wa Global Publishers.
BINTI mwenye miaka 19, Sabrina Gharib, anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo kwenye Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, leo ametinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online.
“Kwa mara ya kwanza nilipoanza kufanya kazi mochwari nilipewa maiti ya bibi, kiukweli nililia sana na sio kwamba nililia kuiona maiti ama kwa uoga bali kwa uzee aliokuwa nao yule bibi, baada ya hapo nikazoea nikawa nahudumia vizuri,’ alisema Sabrina.
“Nilikuwa na marafiki wengi lakini kwa sasa wengi wamenitenga kutokana na kazi ninayofanya,” alisema Sabrina.
“Mwanzoni alipokuwa akitaka kusomea kazi hii ya mochwari nilimkatalia lakini baadaye nikamruhusu, Sabrina ni mtoto pekee kwangu,” alisema mama Sabrina.
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz
