Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akiweka saini kwenye kitabu cha wageni ofisini kwa mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za waandishi Tanzania (UTPC) alipofika kwaajili ya kukabidhi msaada wa komputa na printa kwaajili ya klabu za waandishi wa habari za Geita, Simiyu, Njombe na Katavi.
Mkurugenzi wa NMB nchini Ms. Ineke Bussemaker akitoa machache mbele ya waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya kazi kwa klabu za waandishi wa habari
Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akikabidhi rasmi komputa mpakato kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan.
Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo. Kutoka kushoto waliokaa ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Geita – Daniel Limbe, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan na kutoka kulia ni Meneja wa NMB tawi la Kenyatta road na Meneja wa NMB kanda ya ziwa – Abraham Augustino.
Benki ya NMB nchini imetoa vifaa vyenye thamani ya Tshs Millioni 28 kwa Klabu mpya nne za waandishi wa Habari nchini.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Desktop Computers 16, laptops 4 na printers 4 ambavyo tayari vimekabidhiwa kwa Geita Press Club na vinatarajiwa kuwasilishwa kwa Katavi Press Club , Simiyu Press Club, na Njombe Press Club ambapo kila klabu itapata Desktop Computer 4, Laptop 1 na Printer 1.
NMB imetambua kuwa ni muhimu kusaidia harakati za habari nchini kupitia kuwezesha klabu mpya za waandishi wa habari za mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavi na Njombe.
Huo ni msaada mkubwa kuwahi kutolewa kwa klabu za waandishi wa habari nchini, NMB imetambua umuhimu wa klabu za waandishi wa habari katika kutumia habari katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi hii.
Akiongea katika makabidhiano ya vifaa vya Klabu ya Geita yaliyofanyika mwishoni mwa juma katika Ofisi za UTPC Mwanza
Mkurugezi Mkuu wa NMB Tanzania Ms. Ineke Bussemaker alisema kwamba wanautambua mchango Mkubwa wa UTPC katika sekta ya habari hapa nchini, hivyo baada ya kupokea maombi ya vifaa kutoka UTPC wakaona ni vyema kuwapatia vifaa hivyo, ili waandishi wa habari waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.