×

Nedy Music kuja na Ommy Dimpoz

IMG-20160425-WA0007

Said Seif ‘Nedy Music’

GABRIEL NG’OSHA
MKALI wa Ngoma ya Dayana, Said Seif ‘Nedy Music’ anatarajia kuachia video ya ngoma mpya hivi karibuni ijulikanayo kama Usiende Mbali akiwa amemshirikisha Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Meneja wa Nedy Music, Mubenga alisema kuwa kichupa hicho kimetayarishwa na dairekta kutoka Sauz, Justin Campos wakati audio imetengenezwa Bongo na Nahreel wa The Industry.

“Tumeamua kuja kimataifa, Nedy Music hajawahi kuwaangusha mashabiki wake kuanzia Ngoma ya Nenda Salama, Dayana na sasa Usiende Mbali ambayo ni moja ya ngoma kali kuwahi kutokea katika tasnia ya muziki Bongo,” alisema Mubenga.

Leave a Comment